0
Nikiangalia siasa za Tanzania mwaka huu,nalazimishwa kukumbuka kuhusu nchi ya Kenya mwaka wa 2002 wakati KANU,chama tawala kilichokaa uongozini kwa zaidi ya miaka 40.Wakati huo,chama tawala kilikuwa katika wakati mgumu sana kwa sababu watu walikuwa wamekata tamaa na uongozi wao.Viwanda vingi vilikuwa vimefungwa,dawa hosiptalini  zilikuwa haba,kiwango cha elimu kilikuwa duni nchini,ukosefu wa ajira ulikuwa asilimia zaidi ya 100.

Katika wakati huo,chama tawala cha wakati huo KANU kilikuwa Bw. Uhuru Kenyatta  (Rais wa Kenya wa sasa)ambaye kwa wengi alionekana mchapa kazi katika jitihada zake za kutaka kurudi uongozini kwa sababu kiongozi wake Mr Daniel Arap Moi alikuwa anastaafu.
Bw Uhuru Kenyatta alifanya kampeni kwa juhudi sana,Akaeleza kwa nini yeye anafaa zaidi kwa sababu ya juhudi zake katika utendaji kazi ,ila watu walikuwa wamechoka na uongozi wa chama cha KANU kama walivyochoka sasa hivi na CCM hapa nchini.Hata wakafikiria kwamba hata kama angeingia gharama  za kubadilisha mfumo wa uongozi ungekuwa gharama sana na hangeweza .

Kwa wakati huo,mgombea wa upinzani Bw. Mwai Kibaki ambaye alikuwa ameshawahi kuwa makamu wa Rais katika serikali ya KANU aliingia madarakani baada ya kushinda kura kupitia NARC chama kilichoundwa kupitia muungano wa vyama vidogo vidogo vya siasa kama UKAWA ilivyo sasa.

Matokeo yake,mfumo wa siasa Kenya ukabadilika ghafla,tatizo la umeme likapungua na wawekezaji wakawekeza Kenya tena.viwanda vingi vikafunguliwa ,madawa hosiptalini yakawa yanapatikana.
Hayo yote yalitokana na mabadiliko ya uongozi.Chama kilichoingia madarakani NARC kikawa hakina budi ila kutimiza matakwa ya wananchi.
Kuanzia hapo mambo yote ya Kenya yakabadilika kiuchumi,uwajibikaji wa viongozi ukawa wa kiwango cha juu,idara ya mahakama ikawa inasimamia haki na sio matakwa ya watu  binafsi kama ilivyo sasa hivi.Mishahara ya wafanyikazi wa serikali yakapanda, na wakawa wanalipwa kwa wakati..

Mwaka wa 2013,Bwana Uhuru Kenyatta akagombea tena urais kupitia chama kingine kinachoitwa TNA,matokeo yake akashinda kura kwa kishindo,sasa anaiongoza Kenya na mafanikio yake hadi sasa yanaridhisha.
Ujumbe wangu kwa Dr. John Pombe Magufuli ,sina tatizo nawe,najua wewe ni mchapakazi ila timu yako kidogo kwa sasa mfumo wake si mzuri na kuurekebisha utakuwa tabu.Kwa hivyo hatuna budi kuupumzisha awamu hii.
Na  kwa watanzania wenzangu,tusiogope mabadiliko kwa maisha mazuri hayatakuwa Tanzania bila mabadiliko.


Wenu Mtanzania anayeipenda nchi yake.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top