0
Picha ya Mwai Kibaki wa Kenya akiapishwa kuwa rais 2002
Naandika haya kwa masikitiko makuu,huku nikijiuliza ubaguzi wa kiafya umeanza lini kuwa SERA nchini kwetu.Wote tunasoma taarifa magazetini na mengine tunayasikia kwa majukwaa ya kampeni kuwa tusimchague mgombea fulani eti kwa sababu ANAUMWA au ana ugonjwa fulani.

Nani alisema mtu akiwa mgonjwa hafai kuwa kiongozi katika nchi hii? Ni katiba? na kama ni katiba kipengele hicho kinafaa kuondolewa haraka iwezekanavyo. Nina hakika 100% tumekuwa tukiwachagua viongozi wenye maradhi mbalimbali na hata mengine yasiokuwa na tiba kama vile UKIMWI,CANCER,KISUKARI na mengine mengi na hao viongozi wakaingia bungeni na kufanya kazi zao vizuri bila maradhi yao kuwa kikwazo katika utendeji kazi wao. na sasa hivi nasikitika sana nikisikia mtu akisema au akiandika mtu fulani asichaguliwe kwa sababu ana ugonjwa fulani.Hata wengine wanafanya igizo la  burudani kuhusu hali ya mtu kiafya.

Hii inanifosi mimi kujiuliza,katika sisi wanadamu nani ana uhakika kuwa ataiona kesho au hata lisaa mbele akiwa hai kwa sababu sasa hivi yeye ni mzima kiafya? Watu wengi tu wazima wa afya wanakufa hapa duniani kila dakika na sekunde si kwa sababu wameugua ghafla bali hata katika ajali,mshtuko wa moyo,shinikizo la damu na mengine mengi.Kwa wale wanaokufa,nina hakika na wanasiasa waliochaguliwa wakiwa na afya njema huwa wapo.Kwa hivyo eti kusema tusimchague mgonjwa kwa sababu hana uhakika wa kuishi ni kama kumtukana Mungu.

Hapa duniani tunaishi kwa kupenda kwake Mungu.Wewe leo unafanya kampeni ukiwa mzima.Je ukishachaguliwa upatwe na maradhi yasiotibika utastaafu?

Mimi niwaombe tu watanzania wenzangu tuache hizo sera na kampeni POTOVU na wale wanaoneza hizo propaganda na sera za kipuuzi waomba nao wapuuzwe. Tukumbuke Kenya Rais Mstaafu  Mwai Kibaki alichaguliwa akiwa anaumwa baada ya kupata ajali na Mungu akamjalia akapona na kuongoza nchi ya Kenya kwa miaka 10. Kwa hivyo hali ya mtu kiafya isiwe sababu ya tumchagua au kutomchagua mtu.
picha Mwai Kibaki baada ya Ajali

Post a Comment

 
Top