Huu ni mwaka wa 54 CCM bado iko madarakani na inajitahidi kurudi tena madarakani kwa hali na mali,lakini ukiangalia,wao wakirudi madarakani japo ni Dr Magufuli ndio atakayekuwa rais wa Jamuhuri,itakuwa sera za chama ndio inayomwongoza,ambayo mpaka sasa naamini wongi mmeona matokeo yake.
Siku ya leo sijajipanga kuongelea kuhusu CCM,nimejipanga kuongelea kuhusu faida ya zitakazotokea kama UKAWA au chama kingine kitaingia madarakani.
1. Mfumo wa uongozi utabadilika na kwa sababu UKAWA watataka kuonekana bora,watajaribu kufanya maendeleo angalau,huku wakijaribu kufanya usemi wa vyama na viongozi wa upinzani zisiwe kama utabiri.Ni katika jitihada hizi ndio mtu wa kawaida atafaidi.
2. CCM wanajua mbinu zote za ubadhirifu waliokuwa wanazitumia wakati wa uongozi wao na kamwe hawataruhusu njia hizo za kwao zitumike na chama kingine kikitawala.Katika hali ya kutafuta njia mpya na bunifu zaidi za "kuchakachua" mali za umma,mwananchi wa kawaida atafikiwa na fedha nyingi za maendeleo kuliko inavyofika sasa CCM wakiwa uongozini.
3.Kwa hali ya kawaida ya maisha,huwezi kupata zaidi katika maisha huku unatumia mbinu zile zile ulizokuwa unatumia mwanzoni ukiwa unapata kidogo."For things to change, we must be willing to change something in ourselves ,our country first".Mabadiliko hayaji tu !
4. Ukijaribu kuangalia nchi za hapa Afrika ya Mashariki hususan Kenya,tangu wafanye mabadiliko ya uongozi kutoka chama cha KANU hadi Narc na sasa TNA,wamepiga hatua kubwa sana kisiasa na kiuchumi.Ukijaribu kuangalia kwa makini ni mabadiliko ya kisiasa ndio yalioleta hayo mazuri yote.Sasa hivi viongozi wa Kenya wanajua ukifanya kosa unawajibishwa na sio unaambiwa UJIUZULU kama ilivyokuwa hapa kwetu na hayo yote ni matunda ya mabadiliko ya kisiasa.
5. Nimesikia watanzania wengine wanaogopa mabadiliko kwa hofu kuwa yataleta vita kama Libya.Lakini ukijaribu kufuatilia Libya,vita havikuletwa na mabadiliko bali na wale ambao hawakutaka kukubali kuwa muda wa mabadiliko umefika na siku zote muda wa mabadiliko ukifika huwa haubishi hodi.Mbona mtu hata katika maisha ya kawaida anakuwa anamtegemea mtu kama mama au baba na Mungu anaamua kumchukua huyo mtu na baada ya muda maisha ya waliokuwa wanamtegemea aliyeaga yanaendelea kama kawaida!
TUSIOGOPE MABADILIKO,yana faida na hasara zake ila mara nyingi huwa na FAIDA zaidi .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment